Zaidi ya watu 20 wauawa katika shambulio lililotokea kwenye basi, Nigeria


 Takriban abiria 21, wakiwemo watoto, wameuawa baada ya basi lao kuvamiwa na watu wenye silaha katika jimbo la Sokoto, kaskazini-magharibi mwa Nigeria, polisi imeeleza.


Walikuwa wakisafiri kutoka mji wa Sabon Birni hadi mji wa Isa karibu na mpaka na Niger.


Msemaji wa polisi Sanusi Abubakar aliiambia BBC kwamba wengine kadhaa wanapata matibabu hospitalini kutokana na majeraha ya moto.


Baadhi ya ripoti zinaonesha kuwa idadi ya waliouawa ni karibu 30.


Mmoja wa waliohusika katika kuwasaidia majeruhi alielezea tukio hilo kuwa la "kuogofya" na kwamba wengi wa waathiriwa walishambuliwa kiasi cha kutotambulika.


Shambulio hilo lilitokea Jumatatu jioni lakini taarifa zimepatikana kwa kuchelewa kutokana na huduma duni za mawasiliano katika eneo hilo.


Baadhi ya ripoti zinasema washambuliaji walichoma gari hilo kwa maksudi na kuwachoma watu waliokuwa ndani huku akaunti nyingine ikionesha moto huo uliwashwa kwenye basi hilo kutokana na milio ya risasi ya washambuliaji.


Polisi wanasema wanachunguza mazingira ya shambulio hilo.


Kuwachoma abiria wakiwa hai ndani ya gari lao na watu wenye silaha si jambo la kawaida katika eneo hilo.


Ni mbinu ambayo kwa kawaida hutumika na kundi la wanamgambo la Boko Haram ambalo huendesha shughuli zake zaidi kaskazini mashariki mwa Nigeria.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka