Watupwa Jela Miaka 20 Kwa Kusafirisha Dawa Za Kulevya


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mtwara imewahukumu kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja washtakiwa Athuman Mnyamvi na Ahmad Mohamed baada ya kuwatia hatiani kwa makosa ya kukutwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya heroin kiasi cha kilogramu 211.


Mahakama hiyo imemwachia huru Moureen Liumba baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.


Sambamba na adhabu hiyo, Mahakama imewataka washtakiwa hao kulipa faini ya Sh 14,281,359,750 kwa makosa yote mawili.


Hukumu hiyo ilisomwa Novemba 29, 2021 na Jaji Alphan baada ya ushahidi wa upande wa Jamhuri kuthibitisha pasipo shaka kwamba, watuhumiwa hao wawili walijihusisha na kusafirisha dawa hizo za kulevya.


Pia mahakama imetoa amri ya kutaifishwa gari aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili T 921 BPY ambalo lilitumika kusafirisha dawa hizo kuwa mali ya Serikali pamoja na kuteketezwa dawa walizokamatwa nazo.


Washtakiwa hao walikamatwa na Kikosi Maalumu cha Kupambana na Dawa za Kulevya Januari 12, 2012 mkoani Lindi wakiwa wanasafirisha dawa hizo kwa njia ya mapipa.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka