Watu 12 wamefariki kwa kujinyonga wilayani Wanging'ombe

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe Lauteri Kanoni amesema,wananchi 12 kuanzia January hadi Novemba mwaka huu wamejinyonga katika wilaya hiyo kutokana na wivu wa mapenzi,migogoro ya ardhi na ugumu wa maisha.


Kanoni amebainisha hayo wakati akitoa taarifa ya hali ya ulinzi na usalama mbele ya mkuu wa mkoa wa Njombe, mhandisi Marwa Rubirya wilayani hapo.


Baadhi ya wananchi akiwemo Gisilary Nziku,Selest Mtega na Fred Ezekiel wamesema vifo vya kujinyonga vinachangiwa na msongo wa mawazo ambao unasababisha kuchukua maamuzi magumu na kuwepo washauri wenye umri mdogo kulingana na anaeshauliwa.


Aidha wananchi wamesema kutokomeza tatizo la watu kujinyonga serikali inatakiwa kuweka washauri wa umri tofauti pamoja na viongozi wa serikali za vijiji kumaliza tofauti za mwenye malalamiko kwa wakati pasipo kuchelewesha na kupendelea upande mmoja.


Mchungaji wa kanisa la TAG Melinze Cefania Tweve amesema chanzo cha kujinyonga ni kuwepo roho ya kishetani kwa maana imani za kishirikina na kuwa na uchungu na changamoto zinazojitokeza ikiwemo migogoro ya ndoa, ardhi na matatizo ya kiukoo.


Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Kamishna msaidizi wa polisi Hamis Issa ametaka wananchi kutojichukulia sheria za kujinyonga pindi inapotokea sintofahamu kati yao na kuomba wachungaji kuongeza kasi ya ushauri kwa wananchi ili kupunguza vifo vya kujinyonga Mkoani Njombe



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka