Ulaya yaidhinisha matumizi ya aina mpya ya tiba ya COVID-19
Taasisi ya usimamizi wa dawa ya Ulaya EMA imeidhinisha jana matumizi ya aina mbili za dawa za kutibu maradhi ya COVID-19, pamoja na matumizi ya dharura ya aina ya tatu ya dawa.
Dawa zilizothibitishwa ni Sotrovimab inayozalishwa kwa pamoja na kampuni ya dawa ya Uingereza ya GlaxoSmithKline na Vir Biotechnology ya Marekani. Kulingana na EMA, Dawa hiyo inapunguza hatari ya wagonjwa walio na dalili hatarishi kulazwa hospitalini ama kufariki. Aina ya tatu ya dawa iliyodhinishwa kutumika kwa dharura ni Xeduvy.
EMA pia imeidhinisha matumizi ya dharura ya vidonge vya COVID-19 vya Pfizer na kusema dawa hiyo inaweza kutumika kuwatibu watu wazima walioambukizwa COVID-19 na wasiohitaji Oksijeni, lakini wanaweza kupata dalili mbaya zaidi.
Kinachosubiriwa sasa ni tume ya Ulaya yenye mamlaka ya mwisho ya kuidhinisha matumizi ya dawa hizo.
Comments
Post a Comment