Tetesi za soka Ulaya Jumatano tarehe 22.12.2021
Real Madrid wanamfuatilia kwa karibu kiungo wa kati -nyuma wa England na Liverpool Joe Gomez, 24. (Mail)
Manchester United, Barcelona na Real Madrid zote zinafuatilia kwa karibu winga wa Bayern Munich na Ufaransa Kingsley Coman, 25. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Liverpool wanashindania Saini ya mshambuliaji wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 21 Mnorway Erling Braut Haaland. (Sky Germany)
Everton imekubali mkataba wa pauni milioni 17, kwa ajili ya kiungo wa kati wa nyuma-kushoto wa Dynamo Kiev na Ukraine Vitaliy Mykolenko, 22, na hivyo ukupata njia ya kumuondoa katika the Toffees mlinzi Mfaransa Lucas Digne, 28, huku Newcastle na Leicester zikiwa na nia ya kumchukua. (The Mirror)
Mshambuliaji wa kati wa Manchester United na Ufaransa Anthony Martial, 26, anataka kujiunga na Sevilla kwa mkopo. (Sky Sports)
Manchester United wamewasiliana na River Plate kuhusiana na kusiani mkataba wa pauni milioni 17 kwa ajili ya mshambuliaji Muargentina mwenye umri wa miaka 21, Julian Alvarez. (Ole - in Spanish)
Nahotha wa Chelsea Cesar Azpilicueta, 32, anataka kubaki katika klabu hiyo licha ya Barcelona kuonyesha nia ya kusaini mkataba na mlinzi huyo Muhispania wakati mkataba wake utakapomalizika msimu huu. (The Athletic - subscription required)
Tottenham Hotspur na Roma wanagombania sahihi ya kiungo wa kati wa Hoffenheim na Ujerumani Florian Grillitsch, 26. (Sky Germany)
Manchester United wana nia ya kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya kati wa kati wa Lazio Mserbia Sergei Milinkovic-Savic, 26. (Il Messaggero - in Italian)
Chelsea ilikuwa na dau la pauni milioni 72 kwa ajili ya mlinzi wa Paris St-Germain Marquinhos, 27, ambalo alilikataa msimu huu. (L'Equipe - in French)
Kiungo wa kati- nyuma wa Brazil Marquinhos atasaini mkataba mpya katika PSG hadi mwaka 2026 au 2027. (Fabrizio Romano)
Everton watafanya jaribio la tatu kusaini mkataba na kiungo wa nyuma-kulia wa Rangers na Uskochi Nathan Patterson, 20. (Guardian)
Comments
Post a Comment