Tetesi za soka Ulaya Jumapili tarehe 19.12.2021

 


Juventus wameonesha nia kwa mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 32, huku mustakabali wake ukiwa shakani katika Uwanja wa Emirates baada ya kuvuliwa unahodha.(Tuttosport - in Italian)


Leeds wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Juventus Mmarekani Weston McKennie lakini itagharimu takriban £20m kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23.(Sun)


Mshambulizi wa Manchester United Edinson Cavani ndiye anayelengwa na Barcelona kwenye dirisha la usajili la Januari lakini Barca wanataka kuhakikishiwa kwamba raia huyo wa Uruguay, 34, amepona jeraha lake kabla ya kusaini mkataba. (Sport - in Spanish)



Winga Juan Mata anasalia kulengwa na Barcelona, ​​huku Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 33 akihangaika kucheza katika klabu ya Manchester United.(Star)


Manchester United iko tayari kushindana na Chelsea katika kinyang'anyiro cha kumnunua mlinzi wa Ufaransa Jules Kounde, 23, kutoka Sevilla. (AS - in Spanish)


Newcastle wana nia ya kutaka kumchukua kwa mkopo mshambuliaji wa Manchester United Mfaransa Anthony Martial, 26, mwezi Januari, huku mshambuliaji wa Inter Milan na Bosnia Edin Dzeko, 35, akilengwa mwingine. (Sun)



Mkurugenzi wa michezo wa Paris St-Germain Leonardo hakati tamaa kuhusu nyota wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, kusaini mkataba mpya licha ya kuhusishwa na Real Madrid. Mbappe anaweza kujadili kandarasi ya awali na vilabu nje ya Ufaransa mwezi Januari.(AS, via Sky Sports)


Paris St-Germain wanajiandaa kujaribu azma ya Barcelona kumbakisha kiungo wa kati wa Uhispania Gavi, 17.(El Nacional - in Catalan)


Newcastle wamependekezwa kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham na Uingereza Dele Alli, 25, atakapopatikana kwa mkopo mwezi Januari. (Football Insider)



Mlengwa mwingine wa Newcastle, mlinzi wa Lille na Uholanzi Sven Botman, 21, hana uhakika kuhusu kuondoka kwa mabingwa hao wa Ufaransa mwezi Januari.(90min)


Mkufunzi wa Tottenham Antonio Conte amezungumza na kiungo wa kati wa Inter Milan na Chile Arturo Vidal, 34, kuhusu kujiunga na klabu hiyo ya London. Wawili hao walishinda mataji ya Serie A wakati walipokuwa pamoja Juventus na Inter. (La Tercera - in Spanish)


Napoli wamebainisha orodha ya wachezaji wanaotarajiwa kuwindwa Januari, akiwemo beki wa Tottenham na Colombia Davinson.(Corriere dello Sport - in Italian)


Bayern Munich watajiunga na kinyang'anyiro cha kumnunua fowadi wa Leeds na Brazil Raphinha, 24, msimu ujao wa joto.(TodoFichajes - in Spanish)


Arsenal wana nia ya kutaka kumsajili winga wa Juventus na Uswidi Dejan Kulusevski, 21.(CalcioMercato - in Italian)


Mkufunzi wa Roma Jose Mourinho anamtaka Tammy Abraham, 24, kusaidia kumshawishi mchezaji mwenzake wa zamani wa Chelsea na England Ruben Loftus-Cheek, 25, kuhamia Stadio Olimpico.



Kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 29, "ana ndoto" ya kucheza soka tena baada ya kuondoka Inter Milan, wakala wake amesema.(Mail)


Watford wanamfuatilia mlinzi wa Sampdoria na Gambia Omar Colley, 29, huku mkufunzi wa Hornets Claudio Ranieri akitaka kuimarisha safu yake ya nyuma mnamo Januari.(Tuttomercatoweb - in Italian)



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka