Siku ya ukimwi ulimwenguni, dunia yahimizwa kutolegeza mapambano

 


Shirika la Umoja wa Mataifa linaloongoza juhudi za kutokomeza ukimwi duniani UNAIDS limesema maambukizi ya virusi ya HIV yanazidi kuongezeka huku watu milioni 1.5 wakiambukizwa virusi hivyo mwaka 2020 pekee. 


Shirika hilo kupitia mkurugenzi wake mkuu Winnie Byanyima limeonya kuwa ukimwi bado ni janga na huenda dunia ikakabiliwa na vifo milioni 7.7 vitokanavyo na ugonjwa huo ndani ya miaka 10 ijayo iwapo viongozi hawatotafuta suluhu ya haraka ya usawa katika upatikanaji wa madawa na matibabu ya ugonjwa huo. 


Mtaalamu wa magonjwa ya maambukizo wa Marekani Daktari Anthony Fauci amesema janga la corona limebadilisha mwelekeo wa juhudi za kisayansi za kupambana na ukimwi na kutatiza malengo ya Umoja wa Mataifa ya kutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030. 


Fauci ameuambia mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa, kwamba juhudi za kupambana na COVID 19 pia zimetatiza usambazaji wa madawa ya kupunguza makali ya ukimwi na kuwaweka hatarini watu wanaougua virusi vya HIV vinavyosababisha ukimwi, kuambukizwa virusi vyengine hatari.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka