Serikali Yazindua Mfumo Wa Anwani Na Makazi Mwanza


WIZARA ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imezindua rasmi matumizi ya mfumo wa anwani ya makazi utakaowasaidia wananchi kutambulika kwa urahisi katika maeneo yao na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii kama uokozi katika majanga ya moto, shughuli za kibiashara zitakazo wafikia majumbani lakini zaidi kupunguza migogoro ya ardhi.


Uzinduzi huo umefanywa na Spika mstaafu na Kamisaa wa sensa ya watu na makazi nchini, Anne Makinda na Waziri Dk. Ashatu Kijaju.


Hafla ya uzinduzi huo imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dr. Angelina Mabula (Mbunge wa Ilemela),  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel, katibu tawala mkoa wa Mwanza Ngusa Samike na viongozi wengine ngazi ya mkoa, wilaya, kata na hata mitaa.


Mradi huo ulipoanza  ulifanyika mkoa wa Mwanza katika Halmashauri za wilaya ya Nyamagana na Ilemela na sasa unaendelea kutekelezwa katika halmashauri za Misungwi, Kwimba, Magu, Sengerema, Ukerewe na Buchosa. 


Wilayani Nyamagana mfumo huo umeonekana kufanya vyema zaidi na kufanikiwa kuwafikia zaidi ya wakazi 485,211 na hadi kukamilika mradi umegharimu jumla ya Shilingi Bilioni 1.655


Utekelezaji huu unafuatia agizo la waziri mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa alilotoa katika ukumbi wa Pius Msekwa jijini Dodoma tarehe 14.9.2016 alipokuwa akizindua muongozo wa mfumo wa anwani za makazi.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka