Rais wa Burkina Faso avunja serikali
Rais wa Burkina Faso amemfukuza kazi Waziri Mkuu wake Christophe Joseph Marie Dabiré na kuvunja serikali.
"Kazi ya Waziri Mkuu imesitishwa, serikali inavunjwa," agizo la rais lilisema.
Aidha bado hakuna dalili ya ni lini kiongozi mkuu wa serikali atateuliwa.
Nchi hiyo ya Afrika Magharibi yenye wakazi milioni 20.5, Burkina Faso imekumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya wanajihadi tangu mwaka 2015 ambayo yamewaacha mamilioni ya wakimbizi wa ndani.
Kaboré ameahidi kuleta "usalama na utulivu" nchini humo katika muhula wake wa pili na wa mwisho lakini hadi sasa hajafanikiwa katika kazi hiyo na kusababisha hasira kuongezeka kutoka kwa wananchi.
Comments
Post a Comment