Mkuu wa UN aonya kuhusu vikwazo vya kusafiri ‘vya ubaguzi wa rangi’

 


Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kwa pamoja wamekosoa vizuizi vya kusafiri vilivyowekwa kwa nchi kadhaa za Kusini mwa Afrika kufuatia ugunduzi wa kirusi cha corona aina ya Omicron.


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alionya kwamba vikwazo hivyo vinaweza kusababisha "kusafiri kwa ubaguzi wa rangi", na kuvielezea kama "vibaya sana, vya kuadhibu na visivyofaa" katika kukomesha kuenea kwa aina hiyo ya kirusi.


Alisema Waafrika hawapaswi kuadhibiwa kwa pamoja kwa kushiriki habari za afya na ulimwengu.


Mwenyekiti wa AU Mahamat Faki alisema mataifa tajiri yanapaswa kusaidia bara hilo kuongeza viwango vyake vya chanjo ambayo kwa sasa iko chini ya 6% huku baadhi ya nchi zilizoendelea tayari zikitoa chanjo ya tatu.


Haya yanajiri siku moja tu baada ya Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na mwenzake wa Nigeria kuzitaka nchi kuondoa marufuku ya kusafiri.


Shirika la Afya Ulimwenguni linasema takriban nchi 23 ulimwenguni sasa zimeripoti maambukizi ya kirusi cha Omicron.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka