Meli za mizigo zagongana katika Bahari ya Baltic karibu na pwani ya Uswidi
Meli mbili za mizigo zimegongana katika Bahari ya Baltic karibu na pwani ya Uswidi na kusababisha meli moja kuzama, vyombo vya habari vya Uswidi vimeripoti.
Watu kadhaa wanahofiwa kuwa majini na operesheni kubwa ya uokoaji inaendelea, shirika la utangazaji la umma la Uswidi SVT liliripoti Jumatatu.
Meli moja inasemekana kusajiliwa Denmark na nyingine Uingereza.
Maelezo ya mgongano huo, ikiwa ni pamoja na sababu na ni watu wangapi walikuwa kwenye meli iliyozama, hayajulikani.
Tukio hilo lilitokea katika eneo la Bahari ya Baltic kati ya mji wa pwani ya kusini mwa Uswidi wa Ystad na kisiwa cha Denmark Bornholm, Mamlaka ya Bahari ya Uswidi (SMA) ilisema.
Msemaji wa SMA, Jonas Franzen, alisema meli ya Denmark - Karin Hoej - ilikuwa imepinduka. Inasemekana kuwa meli hiyo ilikuwa na watu wawili.
Meli hiyo yenye bendera ya Uingereza ilitajwa kuwa Scot Carrier.
"Tulipokea ripoti kwamba vilio vilisikika kutoka kwa maji," Bw Frazen alisema.
Alisema ripoti hizo zilikuja karibu 04:45 saa za huko(03:45 GMT) siku ya Jumatatu.
"Bado hatujapata mtu yeyote. Lakini tumeomba rasilimali za kupiga mbizi... kuna giza na baridi sana ndani ya maji," aliongeza.
Helikopta na boti zipatazo 10 kutoka Uswidi na Denmark zimejiunga na juhudi za utafutaji na uokoaji, SVT inaripoti.
Shirika la habari la Uswidi TT lilimnukuu msemaji wa walinzi wa pwani wa Uswidi
Moja ya meli hizo ina urefu wa 90m na nyingine 55m, shirika la habari la Uswidi TT lilisema.
Comments
Post a Comment