Mbunge kujenga shule ya Kata bila michango ya wananchi asema itakuwa shule ya mfano jimboni kwake

 


Na Clavery Christian Bukoba Kagera

Juhudi za serikali kuhakikisha kila kata inakuwa na sekondari zikiwa zinaendelea mbunge wa jimbo la Bukoba vijijini amewaahidi wananchi wa kata ya Rukoma kumalizia ujenzi wa shule ya sekondari ya kata hiyo kikamilifu na kuwa shule hiyo ikikamilika itakuwa ya mfano jimboni humo kwa kuwa itakuwa na miundombinu ya kutosha na ya kisasa.


Mbunge huyo amesema hayo katika mkutano wa hadhara na wanachi wa kata hiyo katika viwanja vya shule hiyo inapojenwa ambapo kwa sasa shule hiyo ina vyumba vitatu vya madarasa vilivyokamilika na vitatu vinaendelea na ujenzi kwa fedha zilizotolewa na serikali ili ifikapo January mwaka kesho wanafunzi waweze kuanza kusomea hapo na wapunguze kutembea umbali mrefu pamoja na kuamka usiku ili kuwai shuleni hali ambayo inaweka maisha yao hatarini kwani njian kuna vichaka vyenye wanyama wakari kama mbwa mwitu na fisi.


Mh. Rweikiza amesema kuwa amesikia kilio cha wananchi na anafahamu ni jinsi gani wanafunzi hao wanatembea umbali mrefu kwenda kata jirani kusoma ambapo amesema changamoto zote hizi ndani ya miezi 12 zitakuwa zimemalizika.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka