Mbunge awakemea vikali wanaoposha kuhusu chanjo ya CORONA

 


Na Clavery Christian Bukoba

Mbunge wa jimbo la Bukoba vijijini Mh. Jassoni Rweikiza amewataka wananchi wa kata ya Kyamuraile, Mugajwale, Kemondo, Rubale na Buendangabo kuacha kusikiliza na kufuata maneno ya watu wapotoshaji wanaowadanganya kuwa chanjo ya UVICO-19 inasababisha madhara katika mfumo wa uzazi na inasumu itawafanya kuwa zezeta endapo watachoma chanjo hiyo.


Mh. Rweikiza amesema katika mikutano yake ya hadhara na wanachi wa kata hizo ikiwa ni ziara yake ya kusikiliza kero na ajenda za wanachi wake waliomchagua kwenda kuwatumikia bungeni kwa kupeleka hoja zao serikalini hili ziweze kutatuliwa kwa kufanyiwa kazi. Ambapo amewataka wanachi kuupuza uvumi huo unaoenezwa na baadhi ya watu kuwa chanjo ya CORONA ina madhara mara moja na kujitokeza kwenda kuchanja ili waweze kujikinga na ugonjwa wa CORONA ambao bado upo unaisumbua dunia kutokana na kubadilika kwake kila mara


‘‘Wazungu hawawezi kutengeneza chanjo kwa mabilioni ya fedha na kuitunza na kuisafirisha kuileta mpaka hapa na gharama za kulipa maprofesa na madaktari ili waje kukua wewe hapo mtu mmoja, kwanza hawakujui na wakitaka kukuua hawawezi kusumbuka kwa kuwa nguo, simu, herein na mikufu mnavaa vitu vyao na hata mkiugua mnatumia dawa zinazotoka kwao mbona hawajawaua?’’ Aliuliza Mh. Rweikiza.


 Mbali na hayo Mh. Rweikiza Mbunge wa jimbo la Bukoba vijijini amewataka wananchi kuenedelea kuwa wavumilivu wakati serikali ya awamu ya 6 ikiendelea kutatua changamoto zao taratibu ikiwemo kuendelea kujenga miradi ya maji na kusogeza huduma ya umeme katika kila kijiji pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa, Zahanati na vituo vya afya pamoja na barabara za mitaa.


Mh. Rweikiza anaendelea na ziara yake jimboni ya siku 8 ikiwa na lengo la kuongea na wanachi wake na kujua shida na hoja zao wanazotaka azibebe na kwenda nazo Bungeni ambapo katika ziara hiyo ameambatana na kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Bukoba (V) na viongo wa idara mbalimbali.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka