Lori la kijeshi lavamia kundi la waandamanaji wa Myanmar huko Yangon


Watu kadhaa wamejeruhiwa baada ya lori la kijeshi kuvamia umati wa waandamanaji katika mji mkuu wa kibiashara wa Myanmar, Yangon.


Walioshuhudia wameviambia vyombo vya habari kuwa wanajeshi hao kisha waliwafyatulia risasi baadhi ya waandamanaji waliokuwa wakikimbia, na kuwapiga wengine.


Tangu mapinduzi ya Februari, zaidi ya watu 1,200 wameuawa wakati wa maandamano na wengine maelfu kufungwa.


Jeshi limesema lilikamata watu 11 katika maandamano hayo. Watatu walijeruhiwa - mmoja yuko katika hali mbaya.


Jeshi halikuthibitisha kama lori lilikuwa limeingia kwenye kundi hilo, lakini lilisema lilitawanya umati wa watu "waliofanya ghasia".


Shirika la habari la eneo hilo MPA lilisema linaamini kuwa waandishi wake wawili walikuwa miongoni mwa wafungwa. Mmoja wao alionekana kujeruhiwa, na walikuwa wamepoteza mawasiliano na mwingine, shirika hilo lilisema.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka