KMC Fc Kuwakaribisha Geita Gold Kesho Dimba La Chamanzi


Kikosi cha Timu ya KMC kesho kitashuka  katika Dimba la chamanzi Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya  mchezo wa  Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara dhidi ya Geita Gold mchezo utakaopigwa saa 16:00 jioni.


Mchezo huo wa mzunguko wa nane  utapigwa kesho huku KMC FC ikiwa mwenyeji na kwamba hadi sasa maandalizi yameshafanyika kwa asilimia kubwa na kikosi kiko tayari kwa mtanange huo.


Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya Kocha Mkuu John Simkoko na wasaidizi wake Habibu Kondo pamoja na Hamad Ally imefanya maandalizi ya kutosha kabisa na kwamba malengo makubwa kwenye mchezo huo ni kuhakikisha kwamba kama Timu inapata ushindi.


Licha ya ushindani uliopo kwa Timu pinzani Geita Gold lakini bado kikosi kinamatumaini makubwa yakufanya vizuri kwenye mchezo wa kesho na hivyo kuondoka na alama tatu muhimu ambazo kila mmoja anazihitaji.


"Kwa ujumla kikosi kipo vizuri, wachezaji wana Afya njema, wanamorali nzuri na kikubwa maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa hivyo tutakwenda kupabambania alama tatu.


 "Maandalizi yetu kwa kiasi kikubwa yamefanyika vizuri, kwasababu tunajua mchezo utakuwa na ushindani mkubwa sana, nasisi tunahitaji matokeo hivyo tutakwenda kupambana ukizingatia KMC ni Timu Bora  nilazima tuendelee kuonyesha ubora wetu.


Hadi Sasa KMC FC imecheza michezo Saba ambapo kati ya michezo hiyo imeshinda mmoja na kupoteza michezo mitatu huku ikitoka sare kwenye  michezo mitatu na kujikusanyia jumla ya alama sita na magoli manne hadi sasa na kuwa kweye nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka