Kirusi cha Omicron huenda kina madhara kidogo ukilinganisha na Delta
Maafisa wa wafya nchini Marekani wamesema wakati kirusi cha Omicron kikionekana kusambaa kwa kasi nchini humo, dalili za awali zinaonyesha kuwa kinaweza kuwa na madhara kidogo ukilinganisha na kirusi cha Delta.
Mshauri mkuu wa afya wa rais Joe Biden, Daktari Anthony Fauci, amekieleza kituo cha CNN kwamba wanasayansi wanahitaji taarifa zaidi kabla ya kuhitimisha juu ya ukali wa Omicron.
Ripoti kutoka Afrika Kusini ambako kirusi hicho kiligunduliwa kwa mara ya kwanza, zinaashiria kuwa kiwango cha watu kuugua hakijaongezeka katika hali ya kutisha.
Fauci alisema utawala wa Biden unazingatia kuondoa marufuku ya safari kwa watu ambao sio raia kuingia Marekani kutoka nchi kadhaa za Kiafrika. Mlipuko wa COVID-19 umeua zaidi ya watu 780,000 nchini Marekani.
Comments
Post a Comment