Kiongozi wa kijeshi Chad sasa ni jenerali kamili

 


Kiongozi wa baraza la kijeshi Chad Mahamat Idriss Déby Itno, amepanda hadi cheo cha juu zaidi katika jeshi, kutoka kwa luteni jenerali hadi jenerali.


Siku ya Jumatano, kiongozi huyo wa Chad alivalia nyota tano kwenye sare yake na bereti alipokuwa akiwasili kwenye ukumbi nje ya ikulu ya rais akiwa na gari la nyota tano.


Hapo awali alikuwa na nyota nne, kama Luteni jenerali.


Mkuu wa itifaki wa rais alituma taarifa kwa vyombo vya habari siku ya Alhamisi kuarifu taasisi za serikali na umma kuhusu mabadiliko hayo.


Mtoto huyo wa kiume wa marehemu kiongozi wa Chad, Idriss Déby Itno, aliingia madarakani baada ya kifo cha babake mwezi Aprili. Baba yake alikuwa rais tangu 1990.


Baba yake pekee ndiye alikuwa na cheo cha jenerali wa kijeshi wa nyota tano kabla ya kifo chake.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka