Hamdok; Utulivu na umoja wa Sudan uko hatarini

 


Waziri Mkuu Abdalla Hamdok amesema utulivu na umoja wa Sudan uko hatarini. Hamdok ametoa wito wa kuwepo kwa makubaliano ya kisiasa, ili kulinda nchi siku zijazo, wakati taifa hilo likiwa limegubikwa na maandamano makubwa ya kupinga mapinduzi ya kijeshi. 


Akizungumza kabla ya maandamano yaliopangwa kufanyika leo Jumapili, kuadhimisha miaka mitatu ya maandamano ambayo yalianzisha vuguvugu maarufu la uasi ambalo lilipelekea kupinduliwa kwa kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir. 


Hamdok amesema Sudan inakabiliwa na kikwazo kikubwa katika mchakato wa mageuzi ambayo inatishia usalama, umoja na utulivu wa nchi, na kulirudisha nyuma taifa hilo. 


Mapinduzi ya Oktoba 25 yalihitimisha ushirikiano uliokuwepo kati ya jeshi na vyama vya siasa vya kiraia baada ya kuondolewa al-Bashir. Vyama hivyo, na kamati za upinzani za mitaa ambazo zimeandaa maandamano makubwa, wamekataa mazungumzo na ushirikiano na jeshi.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka