G7 waionya Urusi iwapo itaivamia Ukraine


Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la mataifa tajiri zaidi ulimwenguni G7 wameionya Urusi kwamba itakabiliwa na hatua kali iwapo itaivamia Ukraine na kuiomba kurejea kwenye mazungumzo. 


Mawaziri hao wametoa onyo hilo, wakati mawaziri wa fedha wa kundi hilo wakitarajiwa kukutana siku ya Jumatatu kutathmini wasiwasi wa kiuchumi, ikiwa ni pamoja na mfumuko wa bei, lakini pia wanatarajiwa kugusia umuhimu wa vikwazo dhidi ya Urusi iwapo itachukua hatua hiyo dhidi ya Ukraine, hii ikiwa ni kulingana na maafisa. 


Katika hatua nyingine rais Joe Biden wa Marekani amesema alimueleza wazi rais wa Urusi Vladimir Putin kwamba taifa hilo litawajibishwa vikali, iwapo itaivamia Ukraine. 


Biden amewaambia waandishi wa habari kwamba upo uwezekano wa Marekani kupeleka wanajeshi wa ardhini nchini Ukraine, kwa kuwa suala la hilo halikujadiliwa hapo awali, ingawa Marekani na vikosi vya kujihami vya NATO vitatakiwa kupeleka wanajeshi zaidi nchini Ukraine ili kuimarisha ulinzi.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka