Billion 2.8 kukamilisha maabara ya Mionzi Kanda ya Ziwa. Na Maridhia Ngemela, Mwanza
Na Maridhia Ngemela, Mwanza
Tume ya nguvu za atomiki Tanzania imeombwa kujikita kwenye utoaji wa elimu ya matumizi ya mionzi kwa wananchi ili waweze kupata uelewa juu ya matumizi Bora na salama.
Ombi hilo limetolewa leo hii na Mh. Omary Kipanga Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia jijini Mwanza kwenye hafla fupi ya uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa maabara ya ofisi ya kanda ya ziwa ya tume ya nguvu za atomiki Tanzania iliyopo katika kata ya Mkolani.
Amesema wananchi wengi hawana uelewa wa matumizi ya Mionzi ni vema wakajikita kutoaelimu ilikuepukana na kuwa na Taifa lenye asali kubwa Sana kutokana na kutokuwa na elimu ya matumizi ya Mionzi.
Pia amewaasa wananchi kuitunza maabara hiyo pindi itakapokuwa imekamilika ili iwezekutoa huduma kwa muda mrefu ambayo itakwenda kupunguza changamoto ya ucheleweshwaji wa vipimo vya mionzi.
Naye Mwenyekiti wa tume za nguvu za atomiki Tanzania Prof.Joseph Msambichaka amesema kuwa mradi wa ujenzi wa maabara ya ofisi ya kanda ya ziwa utagharimu kiasi cha sh bilioni 2.8 hadi kukamilika.
Ameongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo itasaidia sana kurahisha huduma kwa wananchi ukilinganisha na zamani.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya nguvu za atomiki Tanzania Lazaro Busagara amesema kuwa mradi huo unaotekelezwa katika mtaa wa Majengo uliopo Kata ya Mkolani umetoa ajira 100 kwa wakazi wa maeneo hayo.
Prof.Lazoro busagala Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya atomiki Tanzania amesema kuwa, time itakamilisha ofisi za kanda Mwanza, kama mkakati ulivyopangwa ilikuweza kuendelea kutoa huduma hiyo kwa wananchi .
Ameongeza kuwa wataendelea kuwasimamia wakandarasi wawe na umakini zaidi ili jengo liwe bora na time itaendelea kusimamia mradi huo ikamilike kwa muda.
Kwa upande wake muwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Muhandisi Robert Gabriel,ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi amemshukru Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu kwa kuchagua Mkoa wa Mwanza kujengwa maabara hiyo ambayo itakuwa msaada mkubwa kwa nananchi na kuingiza kipato katika Wilaya na mkoa kwa ujumla.
Comments
Post a Comment