Bil 500/- Zatolewa Kuboresha Elimumsingi


NAIBU Katibu Mkuu, Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (anayeshughulikia Elimu), Gerald Mweli amesema serikali imetoa zaidi ya Sh bilioni 500 kwa ajili ya kuboresha Elimumsingi nchini.


Mweli alisema hayo wakati wa ziara yake wilayani Kongwa mkoani Dodoma na kuongeza kuwa kiasi hicho cha fedha kimetolewa kupitia programu mbalimbali za kuimarisha Elimumsingi hapa nchini.


Akifafanua zaidi, Mweli alisema Sh bilioni 304 zimetolewa kupitia mpango wa mapambano na ustawi wa jamii dhidi ya Covid-19 ambapo kati ya hizo Sh bilioni 240 zinajenga vyumba vya madarasa 12,000, Sh bilioni 60 zinajenga vyumba vya madarasa 3,000 kwenye vituo shikizi 907 na Sh bilioni nne zinajenga mabweni 50 ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu. Mweli alisema pia kupitia Programu ya GPE – LANES II na EP4R, serikali imetoa Sh bilioni 113 kujenga miundombinu ya shule za msingi na sekondari nchini.


“Kupitia programu hizo, ujenzi wa shule mpya za msingi 19 na sekondari 15 unafanyika kwa gharama ya Sh bilioni 21.25,” alisema. Mweli alisema kutokana na fedha za tozo za mawasiliano, Sh bilioni saba zimepelekwa kukamilisha maboma ya madarasa 560 ya shule za sekondari yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi ili kuunga mkono jitihada hizo.


Alisema pia Sh bilioni 8.5 za Covid-19 zinajenga miundombinu ya kunawia mikono katika shule za msingi na sekondari.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka