Afisa muuguzi afutwa kazi,mtumishi mwingine kukatwa mshahara 15% kwa miaka mitatu

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Watumishi wawili wa halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe wamekutwa na makosa ya utoro kazini baada ya mashauri yao ya kinidhamu kutolewa uamuzi na baraza la madiwani na kupelekea mmoja kusimamishwa kazi huku mwingine akipewa onyo na kukatwa mshahara wake 15% kwa muda wa miaka mitatu.


Akitangaza maamuzi hayo Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Makambako Salum Mlumbe amewataja watumishi hao kuwa ni Boniface Kyando ambaye ameonywa na kusalia kazini na ofisa muuguzi msaidizi wa zahanati ya kitisi Frank Thomas Selestin akifutwa kazi.


"Tumepitia na tumejiridhisha hatimaye tumetoa maamuzi,Boniface Kyando ni mtendaji wa mtaa wa Golgota kata ya Kitisi huyu anabaki kazini lakini atakatwa mshahara wake asilimia kumi na tano kwa muda wa miaka mitatu kwa kosa la utoro kazini"alisema Mlumbe


Kuhusu Frank alisema "Wa pili ni bwana Frenk Thomas Selestin ambaye ni afisa muuguzi msaidizi daraja la pili katika zahanati ya Kitisi,kosa lake ni utoro kazini tunamfukuza kazi kuanzia leo"


Aidha Makamu mwenyekiti amemtaka mkurugenzi wa halmashauri kukutana na watendaji wote ili kuwakumbusha majukumu yao ya kazi ili watekeleze kwa weledi na halmashauri iweze kufikia malengo waliyojiwekea ikiwemo Ukusanyaji wa mapato.



Awali akitoa salamu za serikali, mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa ameimpongeza  Halmashauri ya mji wa Makambako kwa ukusanyaji wa mapato ya ndani hata hivyo amesisiza kuendelea na mipango itakayowawezesha kufikia malengo makubwa zaidi. 



Akirejea maagizo ya maagizo ya mkuu wa wilaya,Makamu mwenyekiti wa halmashauri amekiri kuwa mapato ndiyo uhai wa halmashauri hivyo amesisitiza ushirikiano baina ya mkurugenzi na madiwani katika kufikia malengo yaliyokusudiwa.




Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka