Posts

Showing posts from December, 2021

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Image
         DOCTOR MBOJE, NI MTAFITI NA MGUNDUZI WA TIBA ASILI YENYE KUTIBU MAGONJWA SUGU NA MWENYE OFU YA MUNGU ANATOBU NA KUPONA KABISA UNABAKI NA ISTORIA MAGONJWA NINAYO TIBU NI  A,_KISUKARI na tibu kwa miti shamba  kunywa na kupona kabisa B,_TEZI DUME_natibu kwa miti  kunywa na kupona kabisa bila kufanyiwa upasuaji C,_NGUVU ZA KIUME    Kwa wale wenye upungufu wa nguvu za kiume na wasio kua nazo kabisa natibu kwa miti shamba na kupona kabisa D,_kutibu magonjwa mbalimbali Kama uzazi) (miguu kuvimba na kuwaka Moto) (Tumbo kujaa gesi na kupata choo ngumu) (mgongo,   kiuno) MHERA JIGURHU ni dawa ya miti shamba inatibu kisukari na kupona kabisa kwa mda wa siku 16  Sukari iwe kubwa kabisa lakini iwe normal 5.1   NNKOROBHIJE ,ni dawa ya miti shamba inayotibu  TEZI DUME bila kufanyiwa operation na kupona kabisa kwa siku 14 na kibaki history  NHUNGHU MAPANDO Kwa wale wenye upungufu wa nguvu...

Vikosi vya Ethiopia vyasema vimesafisha himaya za TPLF

Image
  Serekali ya Ethiopia, Jumanne imesema jeshi lake lilikuwa likisafisha himaya za vikosi vya Tigray katika mikoa ya kaskazini ya Amhara na Afar. Habari hizo zinakinzana na taarifa za Wa-Tigray kwamba vikosi vyake vilijiondoa vyenyewe ili kuweka mazingira mazuri ya kuleta amani. Maelfu ya raia wameuwawa kutokana na vita vya miezi 13 huku wengine 400,000 wakikabiliwa na hali ya ukame katika eneo la Tigray, na watu milioni 9.4 wakihitaji msaada wa chakula kote kaskazini mwa Ethiopia. TPLF chama kinacho tawala Tigray ambacho kipo vitani na serekali, kilitangaza kujitoa katika mikoa ya karibu ya Amhara na Afar Jumatatu. Msemaji wa serekali Billene Seyoum aliwaeleza wanahabari katika mkutano kwamba kama ilivyo shuhudiwa katika wiki za hivi karibuni, vikosi vya taifa pamoja na vikosi shirika kutoka mikoa ya Afar na Amhara vimetwaa miji iliyokuwa inashikiliwa na TPLF.

Tetesi za soka Ulaya Jumatano tarehe 22.12.2021

Image
  Real Madrid wanamfuatilia kwa karibu kiungo wa kati -nyuma wa England na Liverpool Joe Gomez, 24. (Mail) Manchester United, Barcelona na Real Madrid zote zinafuatilia kwa karibu winga wa Bayern Munich na Ufaransa Kingsley Coman, 25. (Mundo Deportivo - in Spanish) Liverpool wanashindania Saini ya mshambuliaji wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 21 Mnorway Erling Braut Haaland. (Sky Germany) Everton imekubali mkataba wa pauni milioni 17, kwa ajili ya kiungo wa kati wa nyuma-kushoto wa Dynamo Kiev na Ukraine Vitaliy Mykolenko, 22, na hivyo ukupata njia ya kumuondoa katika the Toffees mlinzi Mfaransa Lucas Digne, 28, huku Newcastle na Leicester zikiwa na nia ya kumchukua. (The Mirror) Mshambuliaji wa kati wa Manchester United na Ufaransa Anthony Martial, 26, anataka kujiunga na Sevilla kwa mkopo. (Sky Sports) Manchester United wamewasiliana na River Plate kuhusiana na kusiani mkataba wa pauni milioni 17 kwa ajili ya mshambuliaji Muargentina mwenye umri wa miaka 2...

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Image
  Tume ya uchaguzi nchini Libya imeagiza kuvunjwa kwa kamati za uchaguzi nchini humo na kutilia mashaka uwezekano wa kuandaliwa kwa uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mnamo Disemba 24. Ijumaa ya Disemba 24, ndio siku ambayo huenda ingekuwa muhimu kwa Walibya kwani kwa mara ya kwanza wangepata nafasi ya kuchagua Rais wao. Hata hivyo, kuvunjwa kwa kamati hizo za uchaguzi moja kwa moja kunamaanisha kuwa uwezekano wa kufanyika kwa uchaguzi ni mdogo mno. Muda mfupi baada ya tangazo la tume hiyo ya uchaguzi, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL ulitoa taarifa na kuonyesha wasiwasi wake juu ya hali ya usalama katika mji mkuu Tripoli. Ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa nchini Libya umesema kujihami kwa baadhi ya makundi kunatishia kuleta mvutano na kusababisha uwezekano wa kuzuka upya kwa mapigano. Ujumbe huo umeongeza kuwa, mizozo ya kisiasa inapaswa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo. Picha zilizochapishwa mitandaoni zimeonyesha vifaru na malori ya kijeshi katika wilaya...

MAGAZETI YA LEO 22/12/2021

Image
 

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka

Image
  Gari ni kifaa au chombo kinachorahisisha usafiri, lakini kinapaswa kutumiwa kwa tahadhari kubwa. Ajali zinazotokana na magari kuwaka moto, mara kadhaa zimekuwa zikisababisha hasara kubwa au hata kugharimu maisha ya watu. Kwa hakika jambo hili si zuri, hivyo kila dereva au mtumiaji wa gari ni muhimu akachukua hatua za tahadhari mapema ili kukabili tatizo hili. Gari kuwaka moto kunaweza kusababishwa na mambo mbalimbali, fuatilia makala hii kwa karibu ili ufahamu mambo 9 yanayosababisha gari kuwaka moto na jinsi ya kuyaepuka. 1. Kuvuja kwa mafuta Ikiwa gari litavuja mafuta  ni rahisi sana kuwaka moto. Kumbuka mafuta ya gari pamoja na mafuta lainishi (oil) ni rahisi sana kushika moto. Tafiti mbalimbali za ajali zimebaini kuwa kuvuja kwa mafuta ni chanzo kikubwa cha magari kuwaka moto. Ni muhimu kuhakikisha unazingatia matengenezo na ukaguzi wa mara kwa mara wa gari lako ili kubaini kama kuna mahali panapovuja mafuta parekebishwe. 2. Hitilafu ya umeme Gari lina mfu...

Maandamano yasababisha vifo Goma, DRC

Image
Afisa wa polisi na raia wawili wameuwawa wakati wa maandamano katika mji wa goma mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jumatatu, kutokana na kuzorota kwa usalama kwa mujibu wa polisi na asasi ya kiraia. Shirika la habari la Reuters linaripoti kwamba mawe makubwa yaliwekwa barabarani ambapo waandamanaji walikusanyika kukabiliana na polisi katika maandamanao ya kupinga ghasia katika eneo hilo, na inaaminika kuwa ni wapinzani wa vikosi vya usalama kutoka katika taifa jirani la Rwanda na kusababisha hali isiyo ya utulivu. Serekali imekanusha madai kwamba vikosi vya Rwanda vinakwenda kusaidia. Watu wengi wa Goma wamechoshwa na kuongezeka kwa mashambulizi yanayo fanywa na makundi kadhaa yenye silaha katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri ambayo yamesababisha serekali kutangaza hali ya tahadhari licha ya uwepo wa jeshi na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa.

MAGAZETI YA LEO 21/12/2021

Image
 

Fahamu tatizo la kukoroma na jinsi ya kuepukana nalo

Image
  Kukoroma ni tatizo linalowapata watu wengi wakati wanapolala ambalo linaweza kuwatokea watu wa kila umri ingawa hutokea mara nyingi kwa wanaume au watu wanene. Kukoroma huzidi kwa kadri umri unavyoongezeka na asilimia 54 ya watu wazima hukoroma baadhi ya wakati huku asilimia 25 ya wengine wakiwa na tabia ya kukoroma kila wakati. Kukoroma baadhi ya wakati kwa kawaida sio tatizo kubwa na mara nyingi huleta tu karaha kwa mtu anayelala karibu na mkoromaji. Hata hivyo kukoroma huko sio tu kwamba huharibu usingizi wa anayekoroma bali pia huwasumbua na kuwakeresha wanaolala karibu na mkoromaji. Wale wenye tabia ya kukoroma, hukoroma kila wanapolala na mara nyingi huchoka wanapoamka, na watu wa aina hii hushauriwa kumuona daktari na kushauriwa kuhusiana na tatizo hilo. Lakini kabla hatujaendela mbele ni bora tujue kukoroma hasa ni nini au hutokea vipi? Mtu huwa anakoroma pale kunapokuwa na kitu au sababu yoyote itakayoziba kuingia au kutoka kwa hewa mdomoni na katika pua. Kuta za ...

Mamlaka ya Anga Dubai yasimamisha kwa muda safari za ndege kutoka Kenya

Image
  Mamlaka ya Anga ya Dubai imesimamisha kwa muda huduma zote za safari za ndege kwa wasafiri wanaoingia na wanaopitia nchi hiyo kutoka Kenya kwa saa 48 kuanzia Jumatatu saa nne na nusu asubuhi kwa saa za Dubai. Katika maagizo yaliyotolewa Jumatatu, DCAA imesema wateja hawataruhusiwa kusafiri na ndege ya shirika la Emirates mjini Nairobi wakati huu. Wasafiri wanaotokea Dubai kwenda Nairobi hawajaathiriwa na uamuzi huu. DCAA haijatoa maelezo zaidi kwa nini imeahirisha safari za ndege ingawa kumekuwa na wasiwasi juu ya wateja kutoa vyeti bandia vya COVID 19. Decemba 17 Emirates iliahirisha ndege zake zote kati ya Nigeria na Dubai ikijibu uamuzi kama huo uliofanywa na maafisa wa Nigeria ikipunguza safari za ndege kuwa ndege moja tu kwa wiki. Wiki iliyopita Kenya imethibitisha kesi ya kwanza ya maambukizi ya kirusi cha Omicron ambapo Wizara ya Afya ya Kenya Jumamosi litangaza kesi za COVID-19 zimeongezeka kuvuka 2,000.

Mji wa kihistoria wa Lalibela warejea mikononi mwa serikali

Image
  Jeshi la Ethiopia limedhibiti tena mji wa kihistoria wa Lalibela kutoka kwa waasi wa Tigray. Hatua hiyo imekuja huku kukiwa na tangazo la kundi la (TPLF) kwamba linajiondoa katika maeneo yote katika maeneo ya Amhara na Afar. TPLF limesema lilichukua uamuzi huo ili kusafisha njia ya suluhu la amani la mgogoro wake na serikali. Mzozo huo umesababisha mzozo mkubwa wa kibinadamu, huku juhudi za upatanishi za kimataifa hadi sasa zikishindwa. Haijulikani ni lini wanajeshi waliuchukua tena mji wa Lalibela, lakini Naibu Waziri Mkuu Demeke Mekonnen Hassen alitembelea mji huo, huko Amhara, Jumapili. Lalibela, maarufu kwa makanisa yake ya mwamba ambayo yalianza karne ya 12 na 13, iliteuliwa kuwa kituo cha urithi wa ulimwengu cha UNESCO mnamo 1978. Mji huo umebadilishwa mikono mara kadhaa tkati ya serikali na waasi tangu Agosti. Siku ya Jumamosi, serikali ilisema wanajeshi wake wamechukua tena miji mingine kadhaa, pamoja na Weldiya. TPLF imekuwa ikiwaondoa wapiganaji wake k...