Waziri mkuu wa Canada kuzuru Marekani Alhamis
Wiki kadhaa baada ya mipaka kati ya Marekani na Canada kufunguliwa kutokana na kulegezwa kwa kanuni za Covid-19, sasa kiongozi wa Canada waziri mkuu JustinTrudeau anatarajiwa kuzuru Marekani Alhamisi.
Ziara hiyo ni kwa ajili ya mkutano kati ya taifa lake, Marekani na Mexico, ukiwa wa kwanza kufanyika tangu 2016.
Miongoni mwa masuala yanayotarajiwa kuzungumziwa kwenye kikao hicho ni pendekezo la rais wa Marekani Joe Biden na matumizi ya nishati safi, jambo ambalo limezua utata nchini Canada.
Ingawa chama cha Liberal cha Trudeau kinaunga mkono azimio la Biden na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, uchumi wa taifa hilo unaumia hasa baada hatua ya Biden ya kufuta mradi wa bomba la mafuta la Keystone, ambalo lingesafirisha mafuta ghafi yenye thamani ya mabilioni ya dola kutoka magharibi mwa Canada hadi kwenye viwanda vya kusafishia jimboni Texas hapa Marekani.
Jeffrey Collins ambaye ni profesa kwenye chuo kikuu cha Prince Edward Island ameiambia VOA kwamba Canada ingali ina ushawishi mkubwa kwenye mazungumzo hayo kwa kuwa ina madini muhimu yanayohitajika kwenye utumizi wa nishati safi pamoja na kusidia kuleta udhabiti nchini Haiti kutokana na ukaribu wake na taifa hilo.
Comments
Post a Comment