Wananchi Meru wamuomba Rais Samia kuingilia kati mgawanyo shamba la Valeska

 


Wananchi wa Kijiji cha Kwa Ugoro katika Halmashauri ya Meru wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati ugawaji wa shamba la Valeska lililopo katika Halmashauri hiyo kwa madai ya kutoridhishwa na mgawanyo ulivyofanyika.


Wakizungumza baada ya mkutano wa Kijiji hicho wamesema wanashangazwa na agizo la Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandis Richard Ruyango aliloitoa Novemba 18, 2021 katika ziara yake wilayani humo la kuwataka wananchi waliovamia shamba hilo kupisha wataalamu ndani ya siku 14.


Wamedai kuwa katika mgawanyo wa shamba hilo, walitakiwa wapewe eke 2,500 lakini wamepewa 1500 na 2586 kubaki kuwa mali ya Halmashauri hiyo hali iliyowaacha kwenye sintofahamu.


Wakati wananchi hao wakilalamika kupewa eneo dogo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wilium Lukuvi alipofanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru Julai 1, 2021 alitoa maelekezo ya Serikali juu ya upangaji wa shamba la Valeska ikiwa ni pamoja na kuelekeza vijiji vitatu vinavyozunguka shamba hilo kupewa eka 1,500 kwa mgawanyo wa ekari 500 kwa kila kijiji.


Mwenyekiti wa kitongoji cha Yeriko, Elisante Isanja amesema ni vyema Rais Samia akaunda tume ya uchunguzi itakayohakiki na kujidhihirisha wananchi wazaliwa na wanaodaiwa kuwa ni wavamizi.


"Mwanzo tulikuwa vizuri lakini huu ubabaishaji umetokea kwenye halmashauri ili wao wamiliki eneo kubwa hivyo tunamuomba Rais wetu Samia Suluhu asikie kilio chetu angilie kati kwani hapa tulipo hatujui hatma yetu kwani tumepewa siku 14 tuondoke ndani ya shamba," amesema Isanja na kuongeza


ADVERTISEMENT


"Tunasikitika Mkuu wa Wilaya kutuita sisi wavamizi hizo hekari 500 walizotusaidia zitatutosha nini ikiwa wakazi tupo zaidi ya 1000,"amesema Isanja.


Mwenyekiti wa Kijiji cha Kwa Ugoro, Julius Mollel amesema eneo hilo ndiko sehemu yao ya kujipatia riziki akisema wakazi waishio hupo wanategemea kilimo na wamejenga makazi ya kudumu pamoja na baadhi ya waliokuwa ndugu zao kuzikwa hapo.


"Tukiondolewa hatuna pakwenda ikiwa ridhiki tunapata hapahapa," amesema Mwenyekiti huyo.


Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango amesema maelezo hayo sio yake bali yanatoka katika nyaraka za Halmashauri kwani wakati anatoa maelekezo hayo wataalamu wa halmashauri walikuwepo hivyo ni vyema wangehoji hapohapo wakati akitoa maelekezo.


"Mtu anapoona kuna mapungufu anajua pakwenda mimi wajibu wangu nimesoma nyaraka za Serikali na kutekeleza basi ili wajue nitimiza wajibu wangu na anayeona kuna shida wale wahusika wapo katika Halmashauri husika," amesema Mhandis Ruyango.


Mhandis Ruyango amesema kama wameona shida ipo ni vyema wakawatafuta wataalamu wa Halmashauri wakawaeleza, wakumbuke siku 14 bado hivyo watafute njia ya kufanya kwani Serikali yao ipo wazi na wenye hati ya viwanja wathibitishe uhalali wa maeneo yao,"amesema Ruyango.


Mwaka 2008 Serikali ilifuta umiliki wa shamba hilo lililokuwa linamilikiwa na Arusha Cooperative Union Limited (ACU) kutokana na ACU kushindwa kuliendeleza.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka