Wanajeshi wa Sudan wauwawa katika shambulizi la Ethiopia


Wanajeshi sita wa Sudan wameauwa jana Jumamosi, katika shambulio lililofanywa na wanajeshi wa Ethiopia dhidi ya kituo cha jeshi la Sudan karibu na mpaka kati ya nchi hizo mbili. Jeshi la Sudan limeliarifu shirika la habari la Uingereza la Reuters. 


Awali pasipo kutoa ufafanuzi zaidi katika taarifa kupitia mtandao wa facebook, jeshi hilo la Sudan lilisema kuwa makundi ya wanajeshi na wanamgambo yalishambulia wanajeshi wake katika eneo la Al- Fashaga Al-sughra na kusababisha vifo.


Shirika la habari la Reuters halikuweza kumpata msemaji wa serikali ya Ethiopia, Legesse Tulu ili aweze kuzungumzia mara moja juu ya mkasa huo.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka