Vikosi vya usalama Cuba vyazuia maandamano makubwa

 


Vikosi vya usalama vya Cuba vimezuia maandamano makubwa yaliyokuwa yamepangwa kufanyika jana Jumatatu. Polisi walifurika katika mitaa ya Havana na wapinzani mashuhuri wamekamatwa au kuzuiliwa nyumbani kwao ili kuwazuia kufanya mikusanyiko iliyopigwa marufuku. 


Marafiki na wanafamilia walisema waliozuiliwa ni pamoja na kiongozi wa upinzani Manuel Cuesta Morua, kiongozi wa vuguvugu la kutetea haki za wanawake na mumewe Angel Moya ambaye ni mfungwa wa zamani wa kisiasa. 


Mkosoaji mwingine wa serikali, Guillermo Farinas, anazuiliwa tangu Ijumaa, na waandalizi wengi wa maandamano na waandishi wa habari wameripotiwa kukamatwa wakati mtandao wa intaneti ukifungwa.


Waziri wa mambo ya nje wa Cuba Bruno Rodriguez amekejeli operesheni hiyo iliyoshindwa huku serikali ya Kikomunisti ikiishutumu Marekani kwa kutaka kuivuruga Cuba kupitia maandamano hayo yaliyokuwa yakitaka wafungwa wa kisiasa waachiliwe.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka