Utulivu umerejea kwenye mpaka kati ya Poland na Belarus


Hali ya utulivu imerejea kwenye mpaka kati ya Poland na Belarus saa kadhaa baada ya vikosi vya usalama vya Poland kutumia maji ya kuwasha kuwakabili wahamiaji waliokwama upande wa Belarus kisa kilichochea mvutano mpya kati ya pande hizo mbili. 


Ghasia kubwa ilizuka mapema hapo jana baada ya polisi ya Poland kuwarushia maji ya kuwasha wahamiaji walio kwenye mpaka wa Kuznica-Bruzgi moja ya maeneo ambako wahamiaji wamekusanyika wakijaribu kuingia kinyume cha sheria nchini Poland. 


Wizara ya Ulinzi ya Poland ilisema vikosi vyake vya ulinzi wa mipaka vilichukua hatua hiyo kuwadhibiti watu waliokuwa wakirusha mawe na kuituhumu Belarus kuwapatia baadhi ya wahamiaji mabomu ya kutoa machozi. 


Mzozo kwenye eneo hilo uliokuwa ukifukuta tangu majira ya kiangazi umepamba moto mapema mwezi wakati maelfu ya wahamiaji wengi kutoka mashariki ya kati wakiendelea kukusanyika kwenye mpaka huo unazingatiwa kuwa moja ya lango la kuingia kwenye kanda ya Umoja wa Ulaya.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka