Upinzani Cuba wasema maandamano yatafanyika licha ya vitisho


Vikosi vya usalama vya Cuba jana vimeyazingira makaazi ya mwanaharakati kinara wa upinzani kuelekea maandamano makubwa dhidi ya serikali yaliyoitishwa leo Jumatatu. 


Mwanaharakati huyo Yunior Garcia aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa nyumba yake imezingira na maafisa wa usalama wakati akijitayarisha kwenda kufanya maandamano peke yake.


Waandishi wa shirika la habari la AFP wameshuhudia maafisa wa serikali waliovalia mavazi ya kiraia wakiwa wameuzingira mtaa anakoishi Garcia na wengine wakiwa juu ya majengo kwenye mtaa huo wanakoishi Wacuba wenye kipato cha kawaida. 


Licha ya onyo kutoka kwa serikali ya rais Miguel Diaz-Canel, upinzani nchini Cuba umeapa kupuuza vitisho na kuendelea na mipango ya kufanya maandamano makubwa leo kudai haki za kidemokrasia pamoja na kuachiwa huru kwa wafuasi wa upinzani waliokamatwa mnamo mwezi Julai.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka