Ujerumani yakumbwa na hali ya dharura kuhusu COVID-19

 Waziri wa Afya wa Ujerumani Jens Spahn amesema hali ya maambukizi ya virusi vya corona imezidi kuwa mbaya zaidi kuliko wiki iliyopita. 


Akizungumza na waandishi wa habari, Spahn ameongeza kwamba Ujerumani inakumbwa na kile alichokitaja kuwa hali ya dharura ya kitaifa. 


Kauli ya Spahn inajiri mnamo wakati bunge la Ujerumani limeidhinisha masharti mapya yanayolenga kudhibiti maambukitzi ya virusi vya corona.Tayari jimbo la kusini mwa UJerumani Bavaria limeweka vikwazo na kufunga baadhi ya biashara ikiwemo masoko ya Krismasi. 


Mnamo siku ya Ijumaa, Ujerumani ilirekodi maambukizi mapya 52,970, siku moja tu baada ya kurekodi idadi ya juu ya zaidi ya maambukizi 65,000 siku iliyotangulia.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka