Ujerumani yakabiliwa na hali ya dharura kuhusu COVID-19

 


Waziri wa Afya wa Ujerumani Jens Spahn amesema wimbi jipya la visa vya virusi vya corona lilalopiga kote Ujerumani limeitumbukiza nchi katika hali ya dharura, akiongeza kuwa hali sasa ni mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa wiki moja iliyopita. 


Wakuu wa serikali ya shirikisho na wa serikali za majimbo, wamekubaliana kuhusu hatua kadhaa mpya za kudhibiti janga la COVID-19. Miongoni mwa hatua hizo ni kuhimiza haja ya utoaji chanjo kwa wafanyakazi wote hospitalini na kwenye vituo vyote vya kuwauguza wagonjwa. 


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema nchi inakumbwa na hali tete na wakati umewadia wa kuchukua hatua. Jirani ya Ujerumani Austria imekuwa nchi ya kwanza Magharibi mwa Ulaya kutangaza tena hatua za kufunga shughuli zote za kawaida katika msimu huu wa mapukutiko ili kupambana na wimbi jipya la maambikizi ya COVID-19. 


Kansela wa kihafidhina wa nchi hiyo Alexander Schallenberg amesema hatua ya kufungwa shughuli za nchi kwa siku 10, na 20 ikizidi sana, akiongeza kuwa itakuwa lazima kwa kila raia kuchanjwa kuanzia Februari mosi.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka