Ugiriki yafungua vituo viwili zaidi vya kuwazuia wahamiaji
Ugiriki jana imefungua vituo viwili zaidi vya kuwazuia wahamiaji kwenye visiwa karibu na Uturuki kama sehemu ya sera kali za kusimamia wimbi la wahamiaji, hatua ambayo imekosolewa na makundi ya haki za binadamu.
Akiongea hapo jana wakati vituo hivyo katika maeneo ya Kros na Leros vilipofunguliwa, waziri wa uhamiaji Notis Mitarachi alisema kuwa hatua hiyo ilikuwa msingi muhimu wa sera yao kali ya uhamiaji lakini inayozingatia haki.
Mitarachi ameongeza kuwa hatimaye wameushughulikia mzozo ulioanza mwaka 2015 ambao sio Ugiriki wala Ulaya inataka kuufufua.
Mamlaka nchini humo inasema kuwa kambi hiyo itaimarisha hali ya maisha kwa waomba hifadhi na tatizo la mzozo huo wa uhamiaji kwa jamii za eneo hilo lakini makundi ya kutetea haki yameihimiza Ugiriki kutafakari upya kuhusu maamuzi hayo.
Shirika la msaada wa kimatibabu la Medecins Sans Frontieres (MSF) limesema kuwa vituo hivyo ni kama magereza.
Comments
Post a Comment