Tisho la Israeli kushambulia Iran laongezeka - kunani?
Katika eneo la maji ya blu la bahari nyekundu la Israeli, Emirati na Bahraini vikosi vya wanamaji kwa mara ya kwanza baada ya siku chache tu zilizopita vilifanya mazoezi ya pamoja ya operesheni za usalama na meli ya kijeshi ya Marekani.
Yalifuatia mchezo wa kijeshi katika uwanja wa ndege wa jangwani uliopo kaskazini mwa mji wa mwambao wa Israeli wa Eilat mwezi uliopita, ambao ulituma ndege kutoka Israeli na nchi nyingine saba zilizozunguka angani.
Nia hasa ya mazoezi ya aina hiyo ilikuwa ni kutuma ujumbe wa onyo kwa Iran, ambayo hivi karibuni ilifanya mazoezi yake makubwa ya kijeshi.
Lakini yanakuja wakati ambapo wengi nchini Israeli wanahofu kuhusu iwapo nchi hii ndogo inaweza hivi karibuni kuhisi kushinikizwa kuchukua hatua ya peke yake ya kuushambulia mpango wa nyuklia wa Iran kijeshi.
Unaweza pia kusoma:
Serikali imetenga dola bilioni 1.5 (£1.1bn) kuliandaa jeshi la Israeli kwa ajili ya uwezekano wa mashambulio dhidi ya maeneo ya nyuklia ya Iran, na kuna maonyo karibu kila siku kutoka kwa viongozi wa kisiasa na kijeshi.
BBC imekuwa ikitafuta maoni ya waangalizi wa ngazi ya juu wa Iran na wachambuzi kuhusu kile kinachoweza kutokea.
"Israeli haina nia ya vita na Iran, lakini haitairuhusu Iran kuwa na silaha za nyuklia ," afisa wa usalama wa Israeli anasema. "Kutokana na maendeleo ya mpango wa nyuklia wa Iran, tunajiandaa kwa mbinu mbali mbali kulingana na kile kitakachojitokeza, ukiwemo uwezo wa kijeshi."
Hali hii inakuja huku mazungumzo baina ya Iran na mataifa matano yenye nguvu duniani (pamoja na Marekani kwa njia isiyo ya moja kwa moja ) kuhusu kufufuliwa kwa mkataba wa mwaka 2015 wa nyuklia-unaofahamika kama Mpango wa kina wa pamoja wa hatua (JCPOA) - yakikaribia kufufuliwa katika mji mkuu wa Austria Vienna tarehe 29 Novemba.
JCPOA iliweka ukomo wa shughuli za Iran za nyuklia na kufungua mitambo yake kwa ajili ya kuimarishwa kwa ukaguzi ili iweze kuondolewa baadhi ya sehemu ya vikwazo vya kimataifa ilivyowekewa. Hatahivyo mkataba huo ulitelekezwa na aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump mwaka 2018, kwa idhini ya Israeli.
Wakati tarehe ya mazungumzo ya awamu mpya ikiwa imepangwa, Iran ilitangaza kuwa inazalisha kilo 25 za uranium iliyorutubishwa kwa hadi 60% - chini kidogo tu ya kiwango ambacho kitahitajika kwa ajili ya bomu la nyuklia-na zaidi ya kilo 210 zimerutubishwa kwa kiwango cha 20%.
Huku Tehran ikiendelea kusisitiza kuwa nia zake ni za amani, hata wataalamu wa Iran wameelezea kuwa kiwango hicho cha urutubishaji cha juu cha uranium awali kilikuwa kinamilikiwa na mataifa yenye silaha za nyuklia.
"Wairan leo wanakaribia kutengeneza silaha za nyuklia kuliko wakati wowote ule uliopita ," anasema afisa wa usalama wa Israeli. "Ukweli huu una athari kubwa kwa usalama wa taifa la Israeli."
Taasisi za ulinzi za Israeli zinakadiria kwamba kama iwapo Iran iliamua kufanya hivyo, inaweza sasa kukusanya uranium iliyorutubishwa ya kutosha kwa ajili ya silaha za nyuklia katika kipindi cha mwezi mmoja.
Mzozo wa nyuklia wa Iran: Maelezo ya kimsingi:
•Mataifa yenye nguvu duniani hayaiamini Iran: Baadji yan chi zinaamini kuwa Iran inataka nguvu za nyuklia kwasababu inataka kutengeneza bomu la nyuklia - inakanusha hili.
•Kwahiyo mkataba ulifikiwa: Mwaka 2015, Iran nan chi nyingine sita zilifikia makubaliano makuu. Iran ilitakiwa kuwasitisha baadhi ya shugulizake ili kuondolewa kwa adhabu kali, au vikwazo, vinavyouumiza uchumi wake.
•Tatizo liko wapi sasa? Iran ilianza tena kazi za nyuklia zilizopigwa marufuku baada yar ais wa Marekani Donald Trump kujiondoa kwenye mkataba na kuiwekea tena vikwazo Iran. Ingawa kiongozi mpya Joe Biden anataka kujiunga ten ana mkataba huo, kila upande unasema upande mwingine lazima uchukue hatua hiyo kwanza.
Kutengeneza silaha za aina hiyo kutahitaji pia kutengeneza vichwa vya vyuklia ambavyo vinaweza kuwa makombora ya ballistic. Muda wa utengenezaji wa makombora hayo ni vigumu kuukokotoa, lakini baadhi ya wataalamu wanasema inaweza miezi 18 hadi 24.
Israeli ambayo inafikiriwa kuwa ina silaha zake za nyuklia lakini inasiistizarasmi ya utata wa kimakusudi, inaiangalia Irana yenye nyuklia kama tisho kubwa; Iran haitambui taifa la Israeli na maafisa wake mara kwa mara huamini kuwa hatimaye Israeli haitakuwepo.
Huku Marekani na Mataifa ya kiarabu ya huba, ambayo Israeli imeunda ushirika nayo, pia yakipinga suala la Iran kuwa na nyuklia, haiku wazi ni kwa kiwango gani maslahi ya mataifa hayo ya kibinafsi yatawazuwia kuisaidia katika malumbano yoyote ya kijeshi.
Muda unasonga
Mshauri wa zamani wa usalam wa kitaifa wa Israeli Yaakov Amidror, ambaye kwa sasa ni mhadhili katika taasisi ya Jerusalem ya usalama na stratejia , kwanza alionya juu ya hatari za mpango wa Iran wa nyuklia katika miaka ya mwanzo ya 1990, alipokuwa akifanya kazi katika ujasusi wa kijeshi.
Ana tathmini hii kuhusu maendeleo ya hivi karibuni kuhusu mzozo wa Israeli na Iran kuhusu nyuklia.
"Israeli haiwezi kuishi na hali ambapo Wairan wanafikia karibu zaidi na zaidi katika kutengeneza bomu, na itatakiwa hivi karibuni kuchukua hatua ya kuizuwia ," alisema.
"Sioni njia yoyote ile isipokuwa kuipiga bomu, kwasababu, siwaoni Wairan wakisitisha ndoto yao ya kuwa na mwavuli wa nyuklia ambapo chini yake wanaweza hata kuwa wachokozi zaidi ya walivyo sasa.
Israeli imewahi kuchukua hatua mara mbili peke yake kuwaangamiza maadui zake -katika Iraq mnamo mwaka 1981, na mwaka 2007 nchini Syria - ambapo ilipata ulipizaji kisasi ulikuwa wa kiwango cha chini sana.
Lakini wachambuzi wengi wanahoji iwapo ina uwezo wa kuendesha mashambulio magumu kuzuwia mpango wa nyuklia wa Iran ambao umepiga hatua kubwa zaidi, unaojumuisha viwanda vingi vya urutubishaji wa madini ya uranium, vikiwemo vilivyojengwa chini ya ardhi, na iwapo itaweza kumudu athari za hatua itakazozichukua.
"Kila mtu katika Israeli anaelewa fika kwamba shambulio linaweza kusababisha vita vigumu sana kuvitatua ," anakiri Amidror.
Iran aliahidi "kujibu la kushitua" kwa shambulio lolote dhidi yake. Inadhaniwa kuwa inaweza kutumia vikosi vyake yenyewe na kuratibu wanamgambo wenye silaha waliosambaa kote katika kanda hiyo ya Mashariki ya Kati : Hezbollah katika Lebanon, kundi ambalo lina maelfu ya roketi, wanamgambo wa Shia katika Iraq, Vuguvugu la Wahudhi katika Yemen, na wanamgambo wa Kiislam wa Jihad katika ukanda wa Gaza.
Licha ya hatari mbaya zinazoweka kujitokeza, baadhi watu katika Israeli wanakadiria kuwa shambulio la Israeli linaweza kuwa muhimu zaidi, hata kama litarudisha nyuma jitihada mipango ya nyuklia ya Iran kwa miaka michache.
Lakini kile wanachoelezea maafisa bado ni kuboresha amani, suluhu la mazungumzo.
" Ninatumaini kwamba njia ya kidiplomasia itafanikiwa ," anasema Sima Shine, mkuu wa zamani wa utafiti wa shirika la ujasusi la Mossad , "lakini sioni kuwa kuna fursa ya kiwango cha juu kwa sasa."
Utawala wa Rais wa Marekani Joe Biden umetoa pendekezo kwa Iran moja kwa moja kurejea katika "kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa kwa pamoja" na JCPOA, lakini Israeli inapinga hilo.
Mkataba huo unaondoa masharti mengi dhidi ya mpango wa nyuklia wa Iran kufikia mwaka 2025 na haukuiwekea Iran ukomo katika utengenezaji wa makombora yake ya ballistic au kukabiliana na makundi ya wanamgambo wanaoiunga mkono kutoka maeneo yote ya kanda hiyo.
"Tathmini yangu ya msimamo wa Iran ni kwamba haitaki kurudi nyuma," anasema Bi Shine, ambaye anaongoza mpango wa Iran katika taasisi ya Israeli ya masomo ya usalama wa taifa.
"Kile ambacho wangependa kukiona, bila shaka, ni kuondolewa kwa vikwazo na wanaelewa kwamba lazima watatakiwa kulipa kitu fulani ili kupata hilo . Swali ni mahesabu ambayo Iran inayafanya-ni kwa kiasi gani Iran inahitaji kuwa na nafuu ya kiuchumi?"
Hofu yake ni kwamba mazungumzo ya nyuklia yanaweza kuwa ni njia tu ya kusogeza muda, huku nchi ikiruhusu kuendelea kusonga mbele kwa mipango yake ya nyuklia, na kulimbikiza uranium iliyorutubishwa.
Comments
Post a Comment