Saudi Arabia yazuia safari zaidi za mataifa ya Afrika

 


Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudi Arabia imezuia safari za anga kutoka Malawi, Zambia, Madagascar, Angola, Shelisheli, Mauritius na visiwa vya Komoro kutokana na hofu ya kusambaa kwa aina mpya ya viusi vya corona. 


Siku ya Ijumaa, taifa hilo pia lilisitisha safari za kwenda na kutoka Afrika Kusini, Namibia, Botswana, Zimbabwe, Msumbiji, Lesotho na Eswatini. Hatua kama hiyo imechukuliwa na mataifa kadhaa ikiwemo ya hivi karibuni ya Israel ambapo imetangaza kufunga mipaka yake, baada ya tangazo Ujerumani la kugundua aina mpya ya kirusi mjini Munich.


Katika taarifa yake, Waziri Mkuu wa Israel, Naftali Bennett amesema wanasubiri idhini ya serikali, kuzuia safari za nje kwa siku 14, hatua ambayo inaifaneya Israel kuwa taifa la kwanza kuchukua hatua kali ya namna hiyo.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka