RC Mara atoa agizo kwa halmashauri
Mkuu wa mkoa wa Mara, Ally Hapi amezitaka halmashauri kuvishirikisha vyombo vya usalama vya mkoa katika kutoa tenda kwa kampuni.
Agizo hilo amelitoa wilayani Tarime wakati akifanya ukaguzi wa maendeleo ya miradi ya elimu inayotekelezwa na fedha za Uviko-19.
Hapi ametoa agizo hilo baada ya kubaini kuna kampuni moja imepewa kazi ya kujenga madarasa 60 katika halmashauri ya wilaya hiyo ilihali kampuni hiyo inatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya fedha za umma.
Hapi aliagiza uchunguzi dhidi ya kampuni hiyo miezi kadhaa iliyopita.
" Hii kampuni inatuhumiwa kusababisha hasara ya mabilioni hapa Tarime na nilipofanya ziara hapa niliagiza Takukuru wafanye uchunguzi tubaini ukweli sasa hata kabla ya uchunguzi kukamilika tayari nyie mmeipa kazi tena kubwa sasa najiuliza vipi kampuni ikipatikana na hatia mtafanyaje" amehoji Hapi.
Amesema kuwa sio nia ya Serikali kuzichagulia halmashauri kampuni za kufanya nazo kazi lakini pale panapokuwepo na tuhuma ni vema Serikali ikajiridhisha kabla ya kutoa kazi nyingine ili kuepuka hasara inayoweza kujitokeza.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Michael Mtenjele amesema halmashauri ya Wilaya ya Tarime vijijini imepokea zaidi ya Sh2.3 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 116
Comments
Post a Comment