Rais Samia ameondoa urasimu huu kwa miezi 8

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu amesema kwa miezi nane ya serikali ya Awamu ya Sita, wamefanikiwa kuondoa urasimu kwenye mambo mbalimbali ikiwemo vibali vya kazi pamoja na uwekezaji.


Rais Samia ameyasema hayo leo Novemba 28, 2021, wakati akihutubia taifa mbele ya mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwenye viwanja vya Ikulu kufunga kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda.


''Nafarijika kusema jiihada tulizochukua kwa kipindi kifupi cha takribani miezi 8, zimeleta chachu ya kuongezeka uwekezaji na idadi ya ajira zinazotarajiwa kutokana na miradi iliyoandikishwa,'' ameeleza Rais Samia Suluhu.


Kwa upande wa vibali vya kazi amesema, ''Maboresho na jitihada yamepelekea kupungua kwa muda wa upatikanaji wa vibali vya kazi kwa kuondoa urasimu na sasa hata ndani ya siku moja mwombaji anaweza kupata kibali kupitia mfumo wa E-Permit. Mfumo huu pia unaruhusu upatikanaji kibali cha ukaazi katika kadi moja, kabla ya hapo kibali kilikuwa kinachukua miezi 6 au zaidi,''.


Rais Yoweri Museveni yupo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ambapo aliwasili jana Jumamosi Novemba 27, 2021.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka