Rais Macron aongoza mkutano kuhakikisha Libya yafanya uchaguzi Disemba
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anaogoza mkutano wa kimataifa mjini Paris unaolenga kuhakikisha kwamba Libya inashikilia mpango wake wa kufanya uchaguzi mnamo Disemba na kufungua ukurasa mpya katika historia yake.
Uchaguzi wa urais unaotazamiwa kufanyika Disemba 24 pamoja na uchaguzi wa bunge ndilo lengo kuu katika mpango wa Umoja wa Mataifa katika kusaidia kurudisha amani katika nchi hiyo ila kumekuwa na shinikizo wakati ambapo mivutano imerejea tena kati ya kambi zinazohasimiana.
Kuna hofu pia kuhusiana na iwapo pande hizo hasimu zitayakubali matokeo ya uchaguzi jambo ambalo linaweza kuamua mustakabali wa nchi hiyo ambayo imekuwa kituo kikuu cha kuwasafirisha wahamiaji wanaopania kuvuuka bahari ya Mediterenia na kuingia Ulaya. Miongoni mwa wanaohudhuria mkutano huo wa leo ni makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris pamoja na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi.
Comments
Post a Comment