Morrison Aishinda Yanga
Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Masuala ya Michezo (CAS) leo Novemba 22, 2021 imetupilia mbali rufaa ya Yanga na mchezaji wa Simba, Bernad Morrison kushinda kesi yake dhidi ya timu hiyo.
Yanga walipeleka kesi hiyo ‘CAS’ baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya Kamati ya Haki na Maadili na Hadhi ya Wachezaji ya TFF, ambayo ilitoa hukumu kuwa mkataba wa Yanga na Morrison ulikuwa na mapungufu.
Aidha, CAS imemuamuru Yanga kulipa gharama zote za kesi dhidi ya mchezaji huyo na Morrison kuilipa Yanga Dola za Marekani 30,000 alizopewa kama sehemu ya usajili.
Yanga wamekuwa wakisisitiza kuwa Morrison ni mchezaji wao halali. Morrison alisajiliwa Yanga katika dirisha dogo 2019/2020, ambayo aliitumikia kwa miezi kadhaa kabla ya kutimkia Simba.
Comments
Post a Comment