Mbeya yaongoza utoaji chanjo Uviko-19
Mkoa wa Mbeya umetajwa kuwa miongoni mwa mikoa kumi iliyofanya vizuri katika uhamasishaji na utoaji wa chanjo ya Uviko-19.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima leo Jumanne Novemba 30, 2021 ametaja mikoa mingine iliyofanya vizuri kuwa ni Mbeya, Mtwara, Ruvuma, Kilimanjaro, Lindi, Dar es Salaam, Arusha, Pwani, Dodoma na Kigoma
Dk Gwajima amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo amesema kuwa wananchi wanatakiwa waendelee kujikinga kutokana na tishio la wimbi la nne la maambukizi ya Uviko-19.
Aidha Dk Gwajika amesisitiza waganga wakuu wa mikoa, Wilaya pamoja na timu za mikoa kuendelea kufanya ufuatiliaji na kutuma taarifa za wagonjwa kwa watoa huduma ya afya nchini.
Gwajima ametoa maelekezo ya uimarishwaji wa upokeaji wa taarifa kutoka kwa jamii kupitia madawati ya tetesi na kuongeza wigo wa upimaji kwa wahisiwa wa ugonjwa wa huo.
Comments
Post a Comment