Mataifa yaafikiana kuhusu mkaa


Takriban mataifa 200 hapo jana yaliafikiana kuhusu mpango unaolenga kuweka hai shabaha muhimu ya ongezeko la joto duniani, ingawa hata hivyo kulifanyika mabadiliko ya dakika ya mwisho ambayo yameashiria kulegeza msimamo kuhusu matumizi ya makaa ya mawe. 


Nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na mataifa madogo ya visiwa, zilisema kuwa zimevunjwa moyo na mabadiliko hayo yaliochochewa ya kupunguza kwa kiasi badala ya kuachana kabisa na matumizi ya nishati ya mkaa ambayo ni chanzo kikuu cha utoaji wa gesi chafu. 


Katika taarifa, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonia Guterres, amesema kuwa sayari dhaifu ya dunia bado inakabiliwa na hatari kubwa na kwamba bado kuna hatari ya kukumbwa na janga la mabadiliko ya hali ya hewa.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka