Marekani yaahidi kuikabili Iran
Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin ameahidi kuizuia Iran kupata silaha za nyuklia na kukabiliana na kile alichokitaja kuwa 'matumizi yake hatari' ya ndege za mashambulizi zisizohitaji rubani katika eneo la Mashariki ya Kati.
Hayo yanajiri mnamo wakati mazungumzo ya kuufufua mkataba ya wa nyuklia wa Iran yamekwama. Akizungumza nchini Bahrain katika mazungumzo ya kila mwaka ya Manama waziri huyo alionekana kulenga kuwashawishi washirika wake wa Mataifa ya Ghuba, wakati utawala wa rais Joe Biden ukijaribu kufufua mkataba wa nyuklia ambao ulitaka Iran kupunguza urutubishaji wa madini ya Urani kwa sharti la kuondolewa vikwazo vya kiuchumi.
Iran kwa muda mrefu imesisitiza kwamba mpango wake wa nyuklia ni wa amani, ingawa mashirika ya kijasusi ya Marekani na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki yanasema Tehran ilikuwa na mpango wa silaha uliopangwa hadi 2003.
Kauli ya waziri huyo inajiri baada ya masheikh wa mataifa ya Ghuba kuonekana kutilia shaka kujitolea kwa Marekani kudumisha ulinzi kwenye ukanda huo wakati vikosi vya Marekani vikitaka kuongeza juhudi za kukabiliana na changamoto zinazongezeka kutoka China na Urusi.
Comments
Post a Comment