Marekani, Ufaransa zajadili shughuli za jeshi la Urusi nchini Ukraine

 


Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken amefanya mazungumzo na mwenzake wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian kuhusu wasiwasi unaosababishwa na shughuli za jeshi la Urusi ndani na karibu na mpaka wa Ukraine. 


Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Marekani Ned Price amesema katika taarifa kuwa wanadiplomasia hao wawili pia walijadili juhudi za pamoja za kuushughulikia mpango wa nyuklia wa Iran. 


Washirika wa Magharibi wamekuwa wakielezea wasiwasi kuhusu Urusi kuwapeleka wanajeshi wake karibu na mpaka na Ukraine. Jeshi la Ukraine limekuwa katika mgogoro na wanaharakati wanaopigania kujitenga wanaoungwa mkono na Urusi katika mikoa ya Donetsk na Lugansk ambao ulizuka baada ya Urusi kuifanya kuwa sehemu yake rasi ya Crimea mwaka wa 2014. Kiev imesema wanajeshi wawili wa Ukraine waliuawa Ijumaa katika mlipuko mashariki mwa nchi.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka