Marekani kuwekea Nicaragua vikwazo

 


Serikali ya Marekani Jumatatu imetangaza vikwazo vipya dhidi ya maafisa kadhaa kwenye serikali ya Nicaragua. 


Hilo ni kufuatia uchaguzi wa hivi karibuni uliomrudisha tena madarakani rais Daniel Ortega kwa muhula wa nne, wakati marekani ikisema kuwa zoezi hilo kuwa lilikuwa na udanganyifu.


Wizara ya fedha ya Marekani imesema Jumatatu kwamba wizara ya umma ya Nicaragua kabla ya uchaguzi wa Novemba 7 iliwakamata na kuwachunguza wagombea wa urais wakati ikiwazuia baadhi yao kushiriki uchaguzi huo, ikitajwa kuwa hujuma ya demokrasia.


Ripoti imeongeza kusema kwamba hatua hiyo ilimhakikishia Ortega ushindi pamoja na mke wake Rosario Murillo ambaye ni naibu wake. Miongoni mwa maafisa wa ngazi za juu waliowekewa vikwazo ni pamoja na waziri wa nishati Salvador Mansell Castrillo, naibu waziri wa fedha Jose Adrian Chavarria Montenego pamoja na Mohamed Farrara Lashatar ambaye ni balozi wa taifa hilo kwenye mataifa ya mashariki ya kati.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka