Malikah Shabbaz: Mwana wa kike wa Malcom X afariki

 


Malikah Shabazz, mwana wa mwanaharakati wa haki za kibinadamu aliyeuawa Malcom Xalipatikana amefariki siku ya Jumatatu nyumbani kwake Brooklyn, mjini New York, kwa mujibu wa polisi.


Shabbaz mwenye urmi wa miaka 56 , alikuwa kitinda mimba wa wasichana sita wa mwanaharakati huyo maarufuambaye miaka 1960 alipigania kuwezeshwa kwa Wamarekani weusi.


Shabbaz alipatikana akiwa amepoteza fahamumwendo wa 4.40 jioni Alitangazwa kufariki muda mfupi baadaye.


Habari hizo zinajiri siku chache tu baada ya wanaume wawili waliopatikana na hatia ya kumuua Malcolm X, Muhammad Aziz na Khalili Islam kuondolewa makosayamuaji yake na mahakama ya mjini New York.


Mapema mwaka huu , Watoto wa kike wa shujaa huyo waliomba kwamba uchunguzi ufunguliwe upya , wakidai kwamba kuna Ushahidi mpya.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka