Lukashenko aisihi Ujerumani kuchukua wakimbizi
Rais Alexander Lukashenko wa Bularus leo hii ameisihi Ujerumani kuwachukua takribani wakimbizi elfu mbili ambao wamekwama katika eneo la mpaka wa Poland na Belarus akisema idadi hiyo si chochote kwa taifa hilo.
Lukashenko aliwahi kutoa kauli kama hiyo baada ya simu yake hivi karibuni na Kansela Angela Merkel kuhusu mgogoro katika eneo la mpakani.
Lakini kwa mara kadhaa serikali ya mjini Berlin imekataa namna yake ya kushuguhulika mzozo huo.Viongozi wa mataifa ya Ulaya wanasema mzozo huo unasababishwa na Lukashenko ambaye alikasirishwa na Umoja wa Ulaya kwa kukataa kutambua matokeo ya uchaguzi wa 2020 unaobishaniwa uliomwingiza madarakani.
Comments
Post a Comment