Iran, China na Urusi zakutana kabla ya mazungumzo ya nyuklia
Timu ya mazungumzo ya Iran inayoongozwa na Ali Baghali Kani ambayo kwa sasa ipo mjini Vienna, Austria, leo hii imefanya mikutano na wajumbe wa mataifa mengine yanayohusika na Mkataba wa Nyuklia wa Iran, kabla ya kuanza upya kwa mazungumzo ya pamoja juu ya mkataba huo ambao taifa hilo la Kiislamu liliingia na mataifa yenye nguvu duniani mwaka 2015.
Mwanadiplomasia wa Iran, Mohammadreza Ghebi, ameliambia shirika la habari la Iran, ISNA, kwamba timu ya Iran iliwasili mjini Vienna leo hii na kuanza mikutano katika ngazi ya wataalamu ambayo inahusisha viongozi wa timu za majadiliano za Urusi na China pamoja na mratibu wa Umoja wa Ulaya, Enrique Mora.
Comments
Post a Comment