Cop 26: Mafuta zingatio la uchafuzi wa mazingira

 


Mkutano wa Kilele wa Mabadiliko ya Tabia Nchi umemalizika jana Jumamosi kwa makubaliano ambayo kwa mara ya kwanza yalilenga nishati ya mafuta kama kichocheo kikuu cha ongezeko la joto duniani.


Takriban mataifa 200 yaliafikiana kuhusu mpango unaolenga kuweka hai shabaha muhimu ya ongezeko la joto duniani kwa kiwango cha nyuzi joto 1.5 , ingawa hata hivyo kulifanyika mabadiliko ya dakika ya mwisho ambayo yameashiria kulegeza msimamo kuhusu matumizi ya makaa ya mawe.


Mjumbe wa Marekani kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi, John Kerry amesema yalikuwa mazungumzo mazuri na hatimaye mkutano utaidhinisha mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi wa Glasgow.


Mkutano huo uliodumu kwa majuma mawili huko Scotland ulionesha mafanikio makubwa katika utatuzi wa kanuni zinazolisimamia soko la gesi ya kaboni, lakini kuna hatua ndogo katika kushughulikia mataifa yaliohatarini na hasa kuhusu ahadi ya muda mrefu ya ufadhili wa mataifa matajiri katika kukabiliana na athari za kimazingira.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka