'bila kuchanjwa Kenya hupati huduma serikalini'

 


Serikali ya Kenya imepanga maagizo ama masharti mapya mwezi ujao kuzuia wananchi ambao hawajachanjwa kupata huduma za serikali.


Waziri wa afya Mutahi Kagwe alisema watu ambao hawajachanjwa watazuiwa kupata huduma za usafiri wa umma, ndege na treni.


Wakenya watapaswa kuonyesha uthibitisho wa kupatiwa chanjo ili kutembelea Taasisi za serikali za elimu, uhamiaji, kodi na huduma zingine.


Utaratibu huo utaanza kufanya kazi Disemba 21.


Kenya imepanga kuchanja watu milioni 10 mpaka kufikia mwishoni mwa Disemba.


Mpaka sasa ni chini ya asilimia 10% ya watu wamepatiwa chanjo.



Comments

Popular posts from this blog

NINATIBU KISUKARI, PRESHA, TEZIDUME, NGIRI NA NGUVU ZA KIUME

Uchaguzi wa rais nchini Libya uko mashakani

Mambo 8 yanayosababisha Gari kuwaka Moto na Jinsi ya kuyaepuka