Biden na Xi kufanya mkutano kwa njia ya mtandao
Rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa China Xi Jinping leo watafanya mkutano kwa njia ya mtandao ambao kwa sehemu kubwa utagubikwa na mivutano inayoongozeka baina ya madola hayo mawili yenye nguvu.
Maafisa wa Marekani wamesema mkutano wa leo Jumatatu utakuwa nafasi muhimu ya kupunguza ushindani kati ya Washington na Beijing na kutafuta njia kwa mataifa hayo hasimu kufanya kazi pamoja kwenye masuala yenye maslahi kwa pande zote.
Mapema wiki iliyopita rais Xi Jinping ambaye amewahi kuzungumza mara mbili kwa njia ya simu na rais Biden, alionya dhidi ya kurejea mivutano ya enzi ya vita baridi kwenye kanda ya Asia na Pasifiki.
Mahusiano kati ya Marekani na China yamepwaya zaidi katika miaka ya karibuni kutokana na mivutano juu ya masuala kadhaa ikiwemo hatma ya kisiwa cha Taiwan, vikwazo vya biashara pamoja na rikodi dhaifu ya haki za binadamu nchini China.
Comments
Post a Comment