Abiy Ahmed aapa kuwamaliza adui zake wakati UN ikihofu janga la njaa
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameapa kuwaangamiza adui zake katika ujumbe wake wa kwanza kutoka kwenye uwanja wa vita, katika vidio iliyoonyeshwa na vyombo vya habari vya serikali. Abiy amesema katika ujumbe wake kuwa ana uhakika wa kulishinda kundi la waasi la TPLF, na kwamba hawatorudi nyuma hadi pale Ethiopia itakapokuwa huru.
Wakati waasi wa Tigray wakidai kuyadhibiti maeneo makubwa, Jumuiya ya kimataifa imezidi kuwa na wasiwasi juu ya kuongezeka kwa mzozo huo huku mataifa ya kigeni yakiwataka raia wake kuondoka nchini.
Waziri Mkuu Abiy pia amedai kwamba jeshi limeudhibiti mji wa Kassagita na wanapanga kuitwaa tena wilaya ya Chifra na mji wa Burka katika mkoa wa Afar ambao unapakana na mkoa wa Tigray ulio ngome ya waasi.
Comments
Post a Comment